PMO | Mwanzo (original) (raw)

Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa

Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
Waziri Mkuu

Wasifu

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidi Bondia Mtanzania Mchanza Yusuph kitita cha Shilingi Milioni Tano za ‘Knockout ya Mama’ baada ya kuibuka mshindi kwa kutwaa ubingwa wa WBF baada ya kushinda pambano dhidi ya mfilipino, Miel Fajardo, kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidi Bondia Mtanzania Mchanza Yusuph kitita cha Shilingi Milioni Tano za ‘Knockout ya Mama’ baada ya kuibuka mshindi kwa kutwaa ubingwa wa WBF baada ya kushinda pambano dhidi ya mfilipino, Miel Fajardo, kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidi Bondia Salmin Kassim kitita cha Shilingi Milioni Tano za ‘Knockout ya Mama’ baada ya kuibuka mshindi kwa kutwaa ubingwa wa WBF baada ya kushinda pambano dhidi ya mfilipino, Adrian Lerasan, kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimvisha Mtanzania Salmin Kassim Mkanda wa ubingwa wa WBF baada ya kushinda pambano dhidi ya mfilipino, Adrian Lerasan kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi tuzo ya kutambua mchango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwezesha tasnia ya mchezo wa ngumi nchini, kwenye tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua kitambaa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Sukuma linalounganisha vijiji vya Ngh’aya na Lumeji ambalo ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 10 hadi kukamilika kwake, Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, Desemba 21, 2024

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Tuzo kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana ya kutambua mchango wake katika sekta ya Uhifadhi na Utalii, katika hafla ya Uzinduzi wa Tuzo za Kitaifa za Uhofadhi na Utalii zilizofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Mt. Meru jijini Arusha Desemba 20, 2024. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Paramagamba Kabudi

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha John Bill Tendwa, Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo na Kuaga mwili wa marehemu Tendwa kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Desemba 19, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu John Bill Tendwa, Msajili Mstaafu wa Vyama vya Siasa, alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo na Kuaga mwili wa marehemu Tendwa kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Desemba 19, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma, Desemba 5, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 03, 2024 ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile yaliyofanyika eneo la Mwongozo, Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Viongozi wengine walioshiriki Mazishi hayo ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu William Lukuvi, Waziri wa Afya Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na viongozi wa Chama na Serikali. Dkt. Ndugulile alifariki usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024 nchini India ambapo alikuwa akipatiwa matibabu. Pichani, Waziri Mkuu akitupa udongo kwenye kaburi la Dkt. Ndugulile.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo wakati aliposhiriki kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Ndugulile katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam Desemba 02, 2024. Tukio hilo liliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile katika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam, Desemba 02, 2024. Tukio la kuaga mwili wa Dkt. Faustine liliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi na kukabidhi magari na pikipiki za kutoa huduma za chanjo katika Halmashauri mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika Kitaifa Uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma tarehe 01 Desemba 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye ufunguzi wa Kongamano la Tano la Maendeleo ya Biashara na Uchumi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma Novemba 22, 2024. Waziri Mkuu alimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kongamano hilo.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha kitabu cha tafiti za biashara 114 zilizoandaliwa na watafiti mbalimbali wa masuala ya biashara, baada ya kukizindua kwenye ufunguzi wa kongamano la tano la Maendeleo ya Biashara na Uchumi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma Novemba 22, 2024. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Saidi Jafo, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Kennedy Hosea, Mkuu wa chuo cha Elimu ya Biashara Prof. Edda Tandi Lwoga. Waziri Mkuu alimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kongamano hilo.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Kamati ya Wataalamu wa Uchunguzi wa Jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo, baada ya kuizindua katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam, Novemba 21, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha nyaraka ya Tathmini ya Utekelezaji wa afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura Nchini, baada ya kukizindua kwenye mkutano wa pamoja wa Mawaziri na Viongozi wa juu wa Shirika la Afya Duniani kuhusu hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura nchini, uliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, Novemba 21, 2024. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti na kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua muendelezo wa zoezi la uokoaji katika jengo lililodondoka eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam na amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu hadi atakapotolewa mtu wa mwisho aliyekwama kwenye jengo hilo. Novemba 18, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kuongoza waombolezaji kuaga miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Novemba 18, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza waombolezaji kuaga miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Novemba 18, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofunga Mkutano wa Kazi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza La Mawaziri (e-CABINET), kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Novemba 11, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu na Kongamano la Umuhimu wa Amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano hilo lililoratibiwa na Jumuiya ya Waislamu wa SHIA Tanzania, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipongezwa na Wabunge, baada ya kusoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa 17 wa Bunge la 12 Bungeni jijini Dodoma, Novemba 08, 2024.

OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa 17 wa Bunge la 12 Bungeni jijini Dodoma, Novemba 08, 2024.

Previous Next

Naibu Waziri Mkuu

Waziri wa Nchi & Naibu Mawaziri

Katibu Mkuu & Naibu Katibu Mkuu

Hakikisheni mabondia wananufaika na vipaji vyao-Majaliwa

Soma zaidi

Waziri Mkuu aweka jiwe la msingi sekondari ya Mwanza Girls'

Soma zaidi

Waziri Mkuu aagiza TANROADS waongeze kasi ya ujenzi daraja la Simiyu

Soma zaidi

Serikali yakabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa Hanang

Soma zaidi

Sekta ya Utalii ni nguzo muhimu kwa uchumi wa Taifa-Majaliwa

Soma zaidi

Benki ya Dunia, SADC zampongeza Rais Samia utekelezaji miradi ya maend...

Soma zaidi

Dkt. Biteko apongeza Tamasha la Ijuka Omuka

Soma zaidi

Wananchi wa Hanang' wamshukuru Rais Samia

Soma zaidi

Wawekezaji wakaribishwa Kagera

Soma zaidi

Dkt. Biteko asema Kagera bado ina fursa ya kuongeza uzalishaji wa kaha...

Soma zaidi

Uzalendo ndio utalifanya Taifa liendelee kujitegemea, hivyo ni muhimu suala hilo likapewa kipaumbele. Tusikubali kushawishiwa na Mtanzania yeyote anayetumiwa na watu wenye lengo la kutaka kuja kututawala, tusikubali lazima tuendelee kuwa huru na tulinde rasilimali kwa manufaa ya wote.

Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
08th Dec, 2020