Mwasiti amkana Misago, ni baada ya Diamond kumuita ‘muke halali ya Sam’ (original) (raw)
Mwasiti Almas amezungumzia salamu ya pongezi aliyopewa na Diamond Platnumz jana kwenye siku yake ya kuzaliwa iliyovumbua uhusiano usiojulikana kati yake na mtangazaji wa Power Jams ya EA Radio, Sam Misago.
Katika salamu hizo, Diamond aliandika: Happy Birthday Chitty… muke halali ya @Sammisago.”
Hata hivyo Mwasiti amekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Misago.
“Diamond mbona ameniweza,” Mwasiti ameiambia Bongo5. “Sikushangaa yeye kuniwish lakini nimeshangaa response ya watu. In short mimi sijaolewa. Yule (Misago) sio boyfriend wangu, mimi yule ni rafiki yangu, hakuna kitu chochote kinachoendelea. Sam mimi namjua muda mrefu sana, sijawahi kusema mahusiano yangu yoyote lakini nikiolewa nitasema,” ameongeza.
“Sijui Nasib kayatoa wapi haya mambo. Sam sio mwanaume wa kukupa aibu yupo kama wanaume wengine, yule na mimi naamini ana girlfriend wake na mimi na boyfriend wangu, kwahiyo sielewi Nasib kwakweli yaani hili suala limeleta mtikisiko. Nimepigiwa na watu wengi sana. Lakini ukweli ni kuna vitu havifichiki ukivifanya lazima watu watajua tu.”