Chura-sugu (original) (raw)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chura-sugu
Chura-sugu wa GarmanChura-sugu wa Garman
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama) Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni) Ngeli: Amphibia (Wanyama wanaoanza maisha kwenye maji na kuendelea nchi kavu) Nusungeli: Lissamphibia (Amfibia waliopo bado) Oda: Anura (Vyura) Nusuoda: Neobatrachia Familia: BufonidaeGray, 1825
Ngazi za chini
Jenasi 6 katika Afrika: Amietophrynus Frost et al., 2006 Churamiti Channing & Stanley, 2002 Mertensophryne Tihen, 1960 Nectophrynoides Buchholz & Peters, 1875 Poyntonophrynus Frost et al., 2006 Schismaderma Smith, 1849

Vyura-sugu ni aina za vyura wa familia Bufonidae katika oda Anura ambao ngozi yao ina sugu. Wana jozi ya tezi kichogoni zinazochoza sumu ya neva (bufotoxin) ili kuzuia maadui.

Vyura hawa huishi kwa nchi kavu au juu ya miti lakini takriban spishi zote hutaga mayai katika maji. Mayai hayo hutoa ndubwi. Spishi za jenasi Nectophrynoides (vyura-sugu msitu) hazitagi mayai lakini huzaa vyura wadogo, kwa sababu ndubwi wanatoka kwa mayai ndani ya kirijaova cha jike na kukua mpaka vyura.