Festus Ezeli (original) (raw)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Festus Ezeli

Ifeanyi Festus Ezeli-Ndulue (amezaliwa 21 Oktoba 1989) alikuwa mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu kutoka Nigeria. [1]

Festus ni mmoja kati ya watoto watano. [2] Alijihusisha na masomo akaweza kumaliza elimu ya sekondari ya juu akiwa na umri wa miaka 14.

Aliweza kuendelea na masomo huko jijini Yuba, California mwaka 2014. [3]

Alicheza misimu mitano katika Chama cha taifa cha mpira wa kikapu. Alicheza kwenye Chuo cha Vanderbilt Kabla ya kuchaguliwa kama chaguo la 30 kwenye machaguzi ya Chama cha taifa cha mpira wa kikapu kwenye timu ya Golden State Warriors. Ezeli alishinda katika fainali ya mwaka 2015 katika mashindano ya Chama cha taifa cha mpira wa kikapu.

Mara ya mwisho alionekana katika fainali ya mwaka 2016, alistaafu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti katika msimu wa 2017.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-22. Iliwekwa mnamo 2019-12-07.
  2. Katz, Andy (Agosti 9, 2011). "Festus Ezeli continues to learn the game". ESPN. Iliwekwa mnamo Agosti 15, 2011.{{[cite web](/wiki/Kigezo:Cite%5Fweb "Kigezo:Cite web")}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Torre, Pablo S. (Machi 7, 2011). "How Did I Get Here?". Sports Illustrated. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-05-02. Iliwekwa mnamo Agosti 15, 2011.{{[cite web](/wiki/Kigezo:Cite%5Fweb "Kigezo:Cite web")}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Festus Ezeli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.