Kwenzi (original) (raw)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwenzi
Kwenzi maridadiKwenzi maridadi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama) Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni) Ngeli: Aves (Ndege) Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro) Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore) Familia: Sturnidae (Ndege walio na mnasaba na kwenzi)Rafinesque, 1815 Spishi: Angalia katiba
Ngazi za chini
Jenasi 33: Acridotheres Vieillot, 1816 Agropsar Oates, 1889 Ampeliceps Blyth, 1842 Aplonis Gould, 1836 Basilornis Bonaparte, 1850 Cinnyricinclus Lesson, 1840 Creatophora Lesson, 1847 Enodes Temminck, 1839 Fregilupus Lesson, 1831 Gracula Linnaeus, 1758 Gracupica Lesson, 1831 Grafisia Bates, 1926 Hartlaubius Bonaparte, 1853 Hylopsar Boetticher, 1941 Lamprotornis Temminck, 1820 Leucopsar Stresemann, 1912 Mino Lesson, 1827 Necropsar Slater, 1879 Neocichla Sharpe, 1876 Notopholia Roberts, 1922 Onychognathus Hartlaub, 1849 Pastor Temminck, 1815 Poeoptera Bonaparte, 1854 Rhabdornis Reichenbach, 1853 Sarcops Walden, 1875 Saroglossa Hodgson, 1844 Scissirostrum Lafresnaye, 1845 Speculipastor Reichenow, 1879 Spodiopsar Sharpe, 1889 Streptocitta Bonaparte, 1850 Sturnia Lesson, 1837 Sturnornis Legge, 1879 Sturnus Linnaeus, 1758

Kwenzi au kuzi ni ndege wadogo kiasi wa familia Sturnidae. Spishi nyingine zinaitwa kizole au nyangala. Wanatokea Ulaya, Afrika, Asia na Australia. Baadhi ya spishi zimewasilishwa katika Amerika ya Kaskazini, Nyuzilandi na Afrika. Wanapenda kuwa kwa makundi. Spishi nyingi zina rangi ya buluu, pengine pamoja na rangi kali kama nyekundu, machungwa na njano; spishi nyingine ni nyeusi, kijivu au kahawia, pengine pamoja na nyeupe, njano, nyekundu au pinki. Sauti yao ina utata na huiga sauti za mazingira, kama ndege wengine, kamsa za magari na hata msemo wa binadamu. Ndege hawa hula wadudu na matunda hasa, lakini hula nusra kila kitu. Takriban spishi zote hulijenga tago lao katika tundu. Jike huyataga mayai 2-6 meupe au buluu.