Moses Swaibu: Hadithi ya mchezaji wa soka aliyegeuka kuwa mpangaji matokeo - BBC News Swahili (original) (raw)

dx

Chanzo cha picha, Getty Images

Moses Swaibu katika ujana wake, baada ya wazazi wake kutengana, yeye na kaka yake walilelewa na baba yao huko Croydon kusini mwa London.

Akiwa na umri wa miaka 16, katika michezo ya majaribio, alifanya vyema wakati wa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya na Crystal Palace na kupata kandarasi ya mchezaji wa kulipwa.

Wiki chache baada ya siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 18, akiwa na Palace, Swaibu alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi.

Alianza mechi yake ya kwanza Selhurst Park katika kikosi cha kwanza cha Palace miezi mitatu baadaye, akitokea benchi katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Everton ya Ligi Kuu ya Uingereza.

“Akilini mwangu, jambo muhimu zaidi maishani mwangu lilikuwa kuhakikisha kwamba ninaweza kulipia kila kitu,” anasema Swaibu katika mahojiano na kipindi cha BBC.

Swaibu alikuwa mtu wa kati, akiwasiliana kati ya wapanga matokeo na kundi la wachezaji karibu 50, kuandaa mikutano na kusambaza pesa.

https://www.bbc.com/swahili/articles/cp8n438zr21o

Kupanga matokeo

,m

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Swaibu akishinda bao la kichwa 2013 akiwa na Sutton United

Moses Swaibu, aliyewahi kuwa mwanasoka wa kutumainiwa, aliingia katika mojawapo ya kashfa kubwa zaidi za upangaji matokeo katika historia ya soka ya Uingereza.

Alizaliwa na kukulia huko Croydon, London Kusini, maisha ya utotoni ya Swaibu yalijaa changamoto, ikiwa ni pamoja na malezi magumu chini ya baba yake baada ya wazazi wake wakimbizi wa Uganda kutengana.

Swaibu alianza maisha yake ya soka, akicheza kama mlinzi wa vilabu kama Crystal Palace na Bromley. Kipaji chake uwanjani kilimfanya kutambuliwa, ikiwa ni pamoja na kutangazwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Crystal Palace.

Uhusiano wake na upangaji matokeo ulitia doa kazi yake iliyokuwa nzuri, na hivyo kumaliza safari yake ya maisha ya soka kwa fedheha mwaka 2013.

Uhusika wa Moses Swaibu katika upangaji matokeo ulianza alipopigiwa simu na Delroy Facey, mwanasoka mwingine wa zamani, kuhusu fursa ya kutengeneza pesa kupitia kamari kinyume cha sheria.

Alikuwa na uwezo wa kudhibiti matokeo ya mechi na kupata mamilioni kwa makampuni ya kamari ya ng'ambo. Yeye pamoja na mwanasoka mwingine, Delroy Facey walipatikana na hatia ya kula njama ya kutoa hongo kufuatia kesi huko Birmingham.

Wafanyabiashara wawili - Chann Sankaran na Krisna Ganeshan - pamoja na mchezaji kandanda Michael Boateng, pia walipatikana na hatia ya kujaribu kurekebisha michezo ya soka katika kesi ya awali.

Baada ya kutoka gerezani

jk

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Swaibu alitumikia miezi minne ya kifungo chake cha miezi 16 gerezani

Wakati alipokuwa gerezani alitembelewa na binti yake mwenye umri wa miaka miwili, ambaye kuwasili kwake kulikuwa kumempa motisha, au pengine kujihesabia haki.

"Alikuja akiwa anakimbia kwenye ukumbi wa wageni, kama watoto wa miaka miwili wanavyofanya, na akakimbia moja kwa moja kuelekea kwangu," anasema Swaibu.

Baada ya kumaliza kifungo chake, Moses Swaibu alitaka kubadili maisha yake kwa kufanya kazi na Chama cha Soka (FA) ili kutoa taarifa za upangaji matokeo.

Swaibu sasa anatumia muda wake kuwaelimisha wachezaji chipukizi kuhusu hatari za kucheza kamari kinyume na sheria na jinsi ya kuepukana na mitego ile ile iliyompelekea kufungwa.

Yaliyopita yamepita. Tangu kuachiliwa kwake, Swaibu amefanya kazi na shirikisho la soka duniani Fifa, shirika la sekta ya Sport Integrity Global Alliance na Ligi Kuu kuelewa saikolojia na mikakati ya wapangaji matokeo.

Pia anashirikiana na mashirika hayo kutambua na kuwalinda watu ambao wako hatarini kujihusisha na ufisadi.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Seif Abdalla